Matendo Ya Rozari Takatifu

SALA: Sala ndio njia yetu kuu ya kuzungumza na kumfikia Mungu, na ndiyo nguvu ya pekee inayoweza kumwokoa mwanadamu hapa Duniani, "Yesu na Maria"... "Yesu na Maria".
🙏 MATENDO YA FURAHA. (Matendo Ya Rozari Takatifu, matendo ya Furaha...)
1. Tendo la kwanza: Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu.
"Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu"

2. Tendo la pili: Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.
"Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani"

3. Tendo la tatu: Yesu anazaliwa Betlehemu.
"Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara"

4. Tendo la nne: Yesu anatolewa hekaluni.
"Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo"

5. Tendo la tano: Maria anamkuta Yesu hekaluni.
"Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa"

🙏 MATENDO YA UCHUNGU (Matendo Ya Rozari Takatifu, matendo ya Uchungu...)
1. Tendo la kwanza: Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.
"Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi"

2. Tendo la pili: Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.
"Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu"

3. Tendo la tatu: Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu.
"Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi"

4. Tendo la nne: Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu.
"Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu"

5. Tendo la tano: Yesu anakufa Msalabani.
"Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria"

🙏 MATENDO YA UTUKUFU. (Matendo Ya Rozari Takatifu, matendo ya Utukufu...)
1. Tendo la kwanza: Yesu anafufuka.
"Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu"

2. Tendo la pili:Yesu anapaa mbinguni.
"Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni"

3. Tendo la tatu: Roho Mtakatifu anawashukia Mitume.
"Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu"

4. Tendo la nne: Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
"Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri"

5. Tendo la tano: Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni.
"Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema"

🙏 MATENDO YA MWANGA. (Matendo Ya Rozari Takatifu, matendo ya Mwanga...)
1. Tendo la kwanza: Yesu anabatizwa Mto Jordani.
"Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo"

2. Tendo la pili: Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.
"Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya Injili"

3. Tendo la tatu: Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
"Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli"

4. Tendo la nne: Yesu anageuka sura.
"Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu"

5. Tendo la tano: Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia.
"Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine"