Mafungo ni safari ya hija ya kiroho ya muumini yenye malengo ya kuboresha na kuleta uhusiano mzuri kati ya muumini na Mungu wake pamoja na mambo anayoyashughulikia
ili kuyaboresha na kupokea uponyaji. Mafungo yana muundo wa kudai ukimya, hivyo muda wa mafungo hutufanya tuwe watu wapya kiroho na pia kiafya na kuwa watoto safi wa Mungu.
🙏 MUUNDO WA MAFUNGO.
1. Mafungo ya mmoja anayefunga. Hapa mtu hujiandaa na kujitenga na walimwengu kwa mda flani, pia anatakiwa kuchagua neno kutoka katika Biblia
na huweza kuwa na Rozari na maji ya baraka katika kuendesha mafungo yake kikamilifu.
2. Mafungo ya mmoja anayeongozwa na mtu mwingine. Haya ni mafungo kwa ajiri ya kupokea Sakramenti ya kitubio, pia huambatana na kuweka nia maalumu.
3. Mafungo ya jamii au familia inayojiongoza ama kuongozwa na wengine.
🙏 SALA KATIKA KILA MWEZI.
1. January: Mwezi wa jina takatifu la Yesu.
2. February: Mwezi wa Mtakatifu Yosefu.
3. March: Mwezi wa mateso ya Yesu.
4. April: Mwezi wa ufufuko wa Yesu Kristo.
5. May: Mwezi wa mbarikiwa Bikra Maria (Fatima).
6. June: Mwezi wa sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.
7. July: Mwezi wa Damu azizi/takatifu ya Yesu.
8. August: Mwezi wa Bikra Maria kupalizwa mbinguni.
9. September: Mwezi wa Msalaba Mtakatifu wa Yesu.
10. October: Mwezi wa Rozari takatifu.
11. November: Mwezi wa kuombea Roho zilizoko Toharani (Marehemu).
12. December: Mwezi wa utatu mtakatifu wa Yesu.
🙏 MGAWANYIKO WA SALA KILA SIKU.
1. Monday: Kuomba kwa ajiri na kwa njia ya Roho Mtakatifu.
2. Tuesday: Tunasali kuwaomba Malaika walinzi, Malaika wa ibaada, Malaika wa Mungu na Malaika wakuu. Malaika Mikaeli (Malaika mlinzi) kwa ajiri ya nguvu ya Mungu.
Malaika Gabriel (Mpeleka ujumbe) kwa ajiri ya ujumbe wa Mungu. Malaika Raphael(Dawa ya Mungu) kwa ajiri ya kuwapa vipaji vya Mungu.
3. Wednesday: Tunasali kumwomba mtakatifu Yosefu, ni msimamizi wa mahitaji na mlinzi wetu.
4. Thusday: Tunasali na kuabudu Ekaristi Takatifu.
5. Friday: Tunasali kwa njia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu (Litania).
6. Saturday: Tunasali kwa njia ya Mama Bikra Maria (Rozari).
7. Sunday: Tunasali kwa njia na kwa ajiri ya ufufuko wa Yesu Kristo.