Uelewa wa jumla juu ya Imani

🙏 MAANA YA IMANI
1. Imani ni hali ya kuamini au kuwa na hakika juu ya kitu, bila kuwa na uthibitisho wa moja kwa moja. Inahusiana na kuamini katika Mungu, nguvu, au dhana fulani, hata kama huwezi kuona au kuthibitisha wazi. Kadiri ya Maandiko Matakatifu, hususan Waraka kwa Waebrania, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana" (rej. Ebr 1 1:1). Katekisimu ya Kanisa Katoliki inaeleza imani kuwa: ni mwambatano zoa nqfsi ya mtu kwa Mungu: wakati huo huo na bila kutengana ni kukubaZi kwa hiari ukweZi vote ambao Mungu ameufunua.
2. Hivyo, kuamini ni kujikabidhi kikamilifu, kwa uhuru kamili na kwa furaha kwa mpango wa Mungu katika historia. Mfano mzuri tunaupata kwa babu yetu wa imani Abraham (rej. Mwa 12-22) na mama yetu Bikira Maria kwa NDIYO yake (Lk 1 :38), tukitaja kwa uchache tu. Kwa msingi huo, rmani ni mwitikio ambao kwao akili na mioyo yetu inasema NDIYO kwa Mungu Baba na kwa kukiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana. Ndiyo hii inabadilisha kabisa maisha ya mtu, inafungua njia kuelekea utimilifu wa maisha na kuyafanya mapya yaliyojaa furaha na matumaini ya kweli.
3. Imani ni zawadi ya kimungu...Kwanza kabisa, imani ni zawadi ya kimungu, yaani, zawadi kutoka kwa Mungu. Imani si tu ni mwitikio wa kiakili wa mwanadamu kwa kweli fulani kuhusu Mungu bali pia ni tendo ambalo kwalo mtu anajikabidhi kwa uhuru kamili kwa Mungu ambaye ni Baba anayetupenda upeo. Mwanadamu anaweza tu kumwamini Mungu kwa sababu yeye (Mungu) anakuja karibu nasi na kugusa maisha yetu kwa njia ya Kristo kwafumbo Ia umwilisho (rej. Yn 1:14), wakati huo huo Roho Mtakatifu akituwezesha kumpokea Mungu katika nafsi zake tatu.
4. Imani ni fadhila ya kimungu...Tunafundishwa kuwa "Imani ni fadhila ya kimungu ambayo kwayo tunamsadiki Mungu na kila kitu alikichosema na alichotufunulia, na ambacho Kanisa takatifu latutaka tukisadiki, kwa sababu Yeye ndiye Ukweli wenyewe" (KKK 1814). Kwa imani 'mwanadamu hujitoa nafsi yake yote kwa Mungu". Ni kwa sababu hiyo mwamini hutafuta kujua na kufanya mapenzi ya Mungu. "Mwenye haki ataishi l•Na imani". Imani hai "hutenda kazi kwa upendo" (Rum.1:17; Gal.5:6).

🙏 KWARESIMA NI SAFARI YA IMANI
1. Kipindi cha Kwaresima ni kipindi cha siku arobaini za toba, kufunga, kusali, kutafakari na matendo ya huruma. Aidha ni kipindi cha kusafiri kiroho na Kristo Mwokozi wetu, kupitia njia ya imani, ambayo lavayo mwanadamu • anashiriki kuujenga Ufalme wa Mungu, ufalme wa upendo, wa haki na amani. Katika safari ya Kwaresima, Kanisa linatuongoza kwa tafakari na mazoezi yatakayotusaidia kukutana na Bwana Mfufuka aliye jiwe kuu la msingi la Ufalme wa Mungu. Kristo ndiye msingi wa imani yetu, imani ambayo "ni mwaliko wa uongofu wa dhati na ulio mpya kwa Bwana, na Mwokozi pekee wa ulimwengu" (rej. Benedikto XVI, Barua ya Kitume Motu Proprio Porta Fidei, 6). Kwaresima ni mwaliko tuupatao kila mwaka ili kila mmoja wetu aione fursa hii ya kiroho. Ni kipindi cha unyamavu, toba na kuzama ndani ya maisha yetu. Kipindi hiki ni cha neema ambapo kila mmoja wetu anaalikwa kufanya jitihada ya kujiinua na kujichotea neema. Bwana wetu Yesu Kristo anatuambia, "Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni ni kuiamini Habari Njema" (Mk 1:15).
2. Safari ya imani yetu ni ndefu. Katika Agano Ia Kale, ililichukua Taifa la Israeli miaka arobaini kuingia katika Nchi ya Ahadi. Kipindi kirefu ambacho, pamoja na kutawaliwa na matendo makuu ya Mungu, kilitawaliwa pia na vishawishi vingi hata kuwafanya Waisraeli wafikirie mara kadhaa kuiacha safari iliyowaelekeza mbele kwenye Nchi ya Ahadi, na kutamani kurudi nyuma, utumwani Misri. Katika Agano Jipya, ilimchukua Yesu Siku arobaini za kufunga ambamo ndani yake aliishiriki hali yetu ya udhaifu, akitufundisha na kutuonesha njia ya kuvishinda vishawishi na dhambi. Safari hii ya Yesu ya Siku arobaini ilikuwa ni kielelezo cha kipindi cha maisha yetu; maisha yanayoonja raha na karaha, yakidai kupokea yote hayo kuwa jicho Ia uradhi wa moyo unaoongozwa na imani. Ni kwa jicho tu Ia imani ndipo tunapoweza kung'amua umri na mpango wa Mungu hata katika hali zile zisizofurahisha na kupendeza, kwani kwa njia hiyo tunaweza kukaa chini na kutafakari juu ya umaana wa mateso yetu. Mtume Yakobo anatukumbusha kuwa, "kujaribiwa kwa imani yetu huleta saburi" (Yak. 1:3; 1 Pet. 1:7).

🙏 IMANI NA JUBILEI YA MWAKA 2025.
1. Baba Mtakatifu ametangaza kwamba mwaka wa 2025 utakuwa ni Mwaka wa Jübilei, ambao hutokea kila baada ya miaka 25. Kauli mbiu ya Jübilei hiyo Mahujaji wa Matumaini". Ni wazo la Baba Mtakatifu kuwa mwaka huu wa jübilei utakuwa mwaka wa matumaini kwa ulimwengu unaoteseka kutokana na athari za vita, athari zinazoendelea za janga la UVIKO- 19, na mabadiliko ya tabia nchi. Kiti Kitakatifu kilitoa nembo rasmi ya Mwaka wa Jübilei 2025 ambayo tafsiri yake, inaonyesha ubinadamu kutoka Pembe Nne za Dunia ( Tazamajuu ya kijitabu hikİ utazİona hizo pembe nne zimeshikİZİa msalaba) katika kitendo cha kushikamana na Msalaba. Msalaba uko katika umbo la tanga, mojawapo ya ishara za Tumaini la Kikristo linalobeba uhakika wa ushindi wa wema dhidi ya uovu. Matanga ambayo yanajizamisha baharini yakisukumwa na matukio ya maisha. Msalaba unaishia kwa umbo la nanga, ishara nyingine ya matumaini ambayo huleta imani na usalama maishani.
Jubilei maana yake nini.
🙏 Maana halisi ya jübilei tunaipata katika kitabucha Mambo ya Walawi (rej. Wal 25:10f) ambapo Waisraeli wanaambiwa kuwa mwaka wa hamsini ni wa jubilei. Ni mwaka Mtakatifu si tu kwa sababu unaanza, unaadhimishwa na unahitimishwa kwa madhehebu matakatifu, bali pia kwa sababu unachochea utakatifu wa maisha. Huu ni mwaka wa undoleo la dhambi, upatanisho, uongofu na toba ya kisakramenti. Ni kipindi cha kumtafuta Kristo anayetutangazia Habari Njema. "Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka uliokubaliwa na Bwana (rej. Isa 61:1-12, Mk 1:15, Lk 4:18-19) Matunda tarajiwa ya mwaka wa jubilei... Jubilei ni wakati ambao utakatifu wa Mungu hudhihirika zaidi nao hutubadilisha. Katika Mwaka mtakatifu tunaalikwa kusimama imara katika imani juu ya uwepo wa Mungu. Tusimame imara kwani imani huzaa tumaini lisilo tahayarisha (Rum 5:5).[mani itufanye kuwa watumishiImani ndicho chombo pekee cha kuhesabiwa haki tunapo mwamini Bwana Yesu Kristo (Mdo 16:31). Na ni kwa imani katika Kristo na Neno lake tunaweza kumtumikia Mungu kwa ufanisi na "kumpendeza, kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini

🙏 MWALIKO WA UJUMLA WA KUSIMAMA IMARA KATIKA IMANI.
Ili tuweze kusimama imara katika Imani, tunaalikwa kutimiza mambo muhimu yafuatayo:
1. Ikumbukwe kwamba haiwezekani kusimama imara katika imani pasipo maisha thabiti ya sala. Sala ni wajibu wa Iazima siku zote kwa sababu kwa njia ya sala tunamtegemea Mwenyezi Mungu katika maisha yetu yote. Kusali ni wajibu unaotakiwa katika dini zote zenye ukweli kimungu. Kwetu sisi wakristo, kusali ni mapokeo ya tangu Agano la Kale. Katika Agano Jipya Kristo alikuja kukamilisha jadi hiyo kwa Yeye mwenyewe kusali mara kwa mara. Vivyo hivyo anatuasa sisi wafuasi wake kusali mara kwa mara ili tusiingie majaribuni (rej. Mt 26:41).
2. Utii kwa Neno la Mungu...Safari yetu ya kiimani katika Kwaresima tuifanyao kila mwaka haina budi kuimarishwa na Neno la Mungu kama ile ya baba yetu Abrahamu iliyoongozwa na sauti ya Mungu (rej. Mwa 12:14). Utii kwa Mungu huimarisha imani yetu. Nasi kwa kumtii Mungu katika Maisha yetu ya kiimani tutaweza kufika mbinguni.
3. Abraham ni mfano bora wa kusimama imara kiimani kwa familia zetu zote. Nyakati hizi za leo familia zimesongwa na kila aina ya madhila, hususani yatokanayo na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ambayo kama matokeo hasi vimeleta changamoto nyingi za kiimani, kimaadili, kijamii na hata kiuchumi. Yote hayo kwa pamoja yamezalisha kizazi ambacho kadiri siku zinavyosonga mbele, mwanadamu huiacha imani na kuifanya sayansi na teknolojia kama ndio msingi mkuu wa maisha yake. Matokeo yake ni kwamba familia zetu zinazidi kuwa legelege kiimani kwa sababu hazichukuliwi tena kuwa eneo Ia malezi muhimu ya kiimani na kiutu. Malezi ya familia 'yamebinafsishwa' katika tendo Ia kuamini kwamba kila mtu katika familia ana wajibu wa kujilea mwenyewe bila ya msaada wa mwingine kati ya wale wanaounda familia. Katika mazingira ya namna hii, dhana nzima ya familia inapotea na familia inapoteza fursa ya kuwa 'shule ya imani', ambamo wazazi na watoto wangetarajiwa kuwa imara katika Imani na utu wema. Ni kwa sababu hiyo, waraka huu unatuhimiza sote katika familia zetu kuiishi imani yetu licha ya changamoto ziletwazo kwetu na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Familia zinaalikwa kuzingatia kusimama imara katika imani kwa sababu "Imani ni nguzo ya maisha ya mtu hapa duniani, kwani imani inamwezesha mtu kuyapokea magumu na majaribu ya maisha kwa ujasiri na saburi (Ebr 12:1-4).
4. Kuishuhudia Imani...Kuna uhusiano mkubwa kati ya fadhila tatu kuu za kimungu: Imani, matumaini na mapendo. Katika kuziishi fadhila hizi hatuna budi kutambua kwamba fadhila hizi haziachani (Rej. 1 Kor 13:13). "Imani inakua pale inapotiwa katika maisha kama uzoefu wa upendo uliopokelewa na pale inaposhirikishwa kwa wengine kama uzoefu wa neema na furaha. Inatufanya kuzaa matunda, kwa sababu inapanua ndani ya mioyo yetu matumaini na kutuwezesha kuwa na ushuhuda ulio hai; hakika, inafungua mioyo na akili za wale wanaosikiliza na kuuitikia mwaliko wa Bwana wa kushikilia neno lake na wa kuwa wafuasi wake." Imani pia inajenga matumaini na matumaini ni dhihirisho la kile tunachokiamini. Kwa hiyo Mwaka huu wa Jubilei unatualika katika kukua na kuziishi fadhila hizi za kimungu kama wahujaji walio na matumaini.
5. Nuru ya imani imewekwa kwa uthabiti katika huduma ya haki, sheria na amani. Imani inatokana na upendo wa Mungu ambapo maana na thamani ya maisha yetu huwa dhahiri. Maisha yetu yanaangazwa kiasi kwamba yanaingia katika nafsi tatu za Mungu zilizo fumbuliwa kwetu na upendo huo. Nuru ya Imani ina uwezo wa kuimarisha utajiri wa mahusiano ya kibinadamu na kuboresha Maisha ya pamoja.